Channel Avatar

Paulnix Ent @UCnNI392glibLXxLzu_vq-OQ@youtube.com

88K subscribers - no pronouns :c

Welcome to PAULNIX ENT official channel. Paulnix is a Kenyan


Welcoem to posts!!

in the future - u will be able to do some more stuff here,,,!! like pat catgirl- i mean um yeah... for now u can only see others's posts :c

Paulnix Ent
Posted 2 weeks ago

Which mix should I upload next?

7 - 2

Paulnix Ent
Posted 3 weeks ago

Dear Lord I trust only you

18 - 6

Paulnix Ent
Posted 2 months ago

Amejibu MAOMBI. Amejibu Kwa wakati Bwana. Amejibu haja ya moyo wangu . Jamani Yesu amefanya

17 - 2

Paulnix Ent
Posted 3 years ago

16 - 4

Paulnix Ent
Posted 3 years ago

KWA NENO LAKO,NITASHUSHA NYAVU:

Luka 5:5-6 SUV

β€œSimoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;”

Petro alikuwa ana haki ya kukataa kushusha nyavu kwa sababu zifuatazo:-

1) Alikuwa amechoka baada ya kufanya kazi usiku kucha bila kupata kitu

2) Alikuwa na uzoefu wa kutosha linapokuja swala la uvuvi, maana ndio kazi aliyoifanya miaka mingi!

3) Siku zote wamekuwa wakivua usiku na sio mchana, kwa hiyo mchana haukuwa wakati sahihi kuzishusha nyavu!

4) Hakuwa na uhakika na uzoefu wa anayemuambia zishushe nyavu

Lakini pamoja na hayo yote aliamua kulitii NENO LA YESU!

Petro akajibu "lakini kwa NENO LAKO nitazishusha nyavu"

Kitendo cha kuanza kwa kusema "LAKINI", anamaanisha kuwa pamoja na sababu zote nilizonazo za kutozishusha nyavu, hizo sababu zote naziona hazifai na ninaziachilia na ninaamua kufanya kile UMESEMA!

Mara nyingine ni rahisi sana mazingira yetu na uzoefu wetu kutufanya TUSILIANGALIE NENO LILILOACHILIWA LA YESU!

Petro alikuwa amehangaika sana kupata samaki bila mafanikio, mazingira yenyewe yalikuwa hayaruhusu kupata samaki, uzoefu wake ulikuwa unamuhakikishia kwamba hawezi kupata samaki lakini KWA NENO LA YESU ALIPATA SAMAKI!

Kwa hiyo, kwenye hiyo CHANGAMOTO inayoonekana kushindikana, unachohitaji ni NENO LA YESU TU JUU YA HIYO CHANGAMOTO!

Uzuri ni kwamba NENO LA YESU LINA UWEZO HATA WA KUUMBA VISIVYOKUWEPO; kwa hiyo sio shida hata kama hicho kitu hakipo kabisa kinaweza kuumbwa na kikawa!

Regard:paulnix ent

24 - 11