Channel Avatar

Msasa Media @UCdz-eU2vUdcd_1JiliLECAg@youtube.com

195K subscribers - no pronouns :c

KANUNI NA MUONGOZO Msasa Media ni Chombo Cha Habari kwa nji


Welcoem to posts!!

in the future - u will be able to do some more stuff here,,,!! like pat catgirl- i mean um yeah... for now u can only see others's posts :c

Msasa Media
Posted 1 week ago

#MsasaUpdates
Mkuu wa kitengo cha Maudhui @msasaonline_ yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam Bw. Godson Mbilinyi @godson2nyi ametembelea kituo cha @vot_media jijini Mwanza kwa lengo la kubadilisha uzoefu wa masuala ya kihabari.

Ziara hii fupi inakuja baada @godson2nyi kukamilisha mafunzo ya Siku 3 juu ya masuala ya Gender Responsive Reporting yaliyofanyika Malaika Resorts Mwanza yakitolewa na School of Media and Communications iliyo chini ya Chuo Kikuu Cha Agha Khan Nairobi Kenya.

Aidha Godson amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na kituo hiki.

#MsasaKisasaZaidi.

111 - 1

Msasa Media
Posted 1 week ago

#MsasaUpdates
MSANII QJ AOKOKA KWA MARA NYINGINE TENA...

Mwanamuziki Mkongwe wa Bongo Fleva aliyebarikiwa sauti ya kipekee kutoka kundi la Wakali Kwanza QJ ameripotiwa kuokoka tena kwa mara nyingine baada ya kuokoka Mwaka 2010 na badae kudaiwa kurudi kwenye matumizi ya Pombe Mwaka 2015 ambapo Kwa mujibu wa Mchungaji Kabigumila ameeleza haya kupitia ukurasa wake wa Instagram

"KUNDI LA BONGO FLEVA WAKALI KWANZA
MWAKA 2004 HADI 2009
Kundi hili liliundwa na vijana watatu wenye vipaji vikubwa vya kuimba Joslin, Makamua na QJ,
Walifanya hit song nyingi za muziki huo na kubwa kuliko zote ilikuwa NATAMANI,
Kwenye wimbo huu kijana aitwaye JOSEPH KELVIN MAPUNDA A.K.A QJ anaimba ubeti huu chini;

Mtoto anang'ara kama candle light, Ana face nzuri ya Kiafrika, Killer boy, Kenya boy, MJ wanamjuaaaa, Uzuri wake hafanani na waridi ama ua poriiiii poriii,

Huyu QJ mwenye mashairi haya na SAUTI YA AJABU YA KUSISIMUA, aliokoka mwaka 2010 kanisa la TFC chini ya Askofu Malasi, akasimama, lakini mwaka 2015 aliondoka na kwa kukosa malezi sahihi ya kiroho akaanza tena ULEVI WA POMBE,

Wiki iliyopita Mungu alinisukuma kutafuta namba yake hadi nikaipata, na kumbe alisharudi kwao kijijini huko wilaya ya Mbinga kwa mama yake, lakini akiwa bado anasumbuka na kunywa japo si kwa kasi ile ya mwanzo!

Nikampata kwa simu, nikaongea naye na kumtumia nauli aje Dar, kwa ruhusa ya mama yake na baba yake mdogo JUMAPILI HII ILIYOPITA YA 01.09.2024 ΑΚΑAFIKA NA AKAFUNGULIWA UPYA, NA MUNGU AKANIAGIZA NIMLEE AWE MCHUNGAJI AMTUMIE KUVUNA KIZAZI HIKI CHA BONGO FLEVA NA WALIONASWA KWENYE WAVU WA MUZIKI WA KIDUNIA!"

#MsasaHabariSaa24

120 - 5

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

#MsasaTrending
NATAMANI TUNGEKUTANA MAPEMA - JUMA JUX...
www.msasamedia.com

585 - 6

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

BISKUTI ZA BURE SHULENI ZASHITUKIWA, MZUNGU ANAGAWA KWA WASICHNA TU...
www.msasamedia.com

84 - 1

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

#MsasaUpdates
MTENDAJI WA KATA AHUKUMIWA BAADA YA KUOMBA RUSHWA...
www.msasamedia.com

37 - 0

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

#MsasaUpdates
UKRAINE YAPIGA MARUFUKU MAKANISA YOTE YENYE UHUSIANO NA URUSI...
www.msasamedia.com

26 - 1

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

#MsasaUnUsual
NYANGUMI ANAYEDHANIWA KUIFANYIA UPELELEZI URUSI AFARIKI DUNIA NCHINI NORWAY....

NA VENANCE JOHN

Nyangumi ambaye ni jamii ya beluga aliyekuwa anadhaniwa kutumiwa na Urusi kwa shughuli za ujasusi (upelelezi) amepatikana akiwa amekufa katika Pwani ya Norway.

Nyangumi huyo alionekana kwa mara ya kwanza katika maji ya Norway miaka mitano iliyopita, akiwa amefungwa kamera.

Nyangumi huyo aliyepewa jina la utani la “Hvaldimir” inasemekana alipewa mafunzo ya kufanya upelelezi (ujasusi) na Urusi.

Mwili wa Hvaldimir umepatikana ukielea karibu na mji wa Risavika, mji ambao uko Kusini Magharibi mwa Norway na Nyangumi huyo amepelekwa bandarini kwa ajili ya uchunguzi.

Shirika la ujasusi la ndani la Norway, liliwahi kusema kwamba kuna uwezekano nyangumi huyo amefunzwa na jeshi la Urusi kwani alionekana kuwazoea wanadamu.

Urusi ina historia ya kutoa mafunzo kwa mamalia wa baharini (viumbe wa baharini) kama vile pomboo (dolphin) kwa madhumuni ya kijeshi ingawa hata hivyo Urusi haijawahi kujibu rasmi madai kama Hvaldimir alipewa mafunzo na jeshi lake.

#MsasaHabariSaa24

22 - 1

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

‪@officialbabbi‬ FT CHRISTIAN BELLA SUPER WOMEN
https://youtu.be/HLCcAZM7k0I?si=Cmu3y...

3 - 0

Msasa Media
Posted 2 weeks ago

NANDY KATIKA UBORA WAKE....

759 - 33

Msasa Media
Posted 1 month ago

#MsasaSports
FULL TIME #CAFCL
VITAL O 0 - 4 YANGA SC

Dube 1
Chama 1
Mzize 1
Aziz Ki 1

#MsasaKisasaZaidi

313 - 1