Channel Avatar

Kikosi kazi cha injili🎖 @UC_8kqo8QcC2Y1F07ZcpdbUA@youtube.com

95K subscribers - no pronouns :c

Unaweza ukawasiliana nasi kwa namba za simu +255769015164 &


Welcoem to posts!!

in the future - u will be able to do some more stuff here,,,!! like pat catgirl- i mean um yeah... for now u can only see others's posts :c

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 week ago

WALIKOKOKA NA KUMAANISHA KWA MUNGU NI WAJINGA SANA

Wasiokoka huwa wanatuona tuliokoka na "KUMAANISHA sana KWA MUNGU" ni wajinga. Sababu yao kubwa huwa wanasema tunakosa RAHA za kidunia.

Ni kweli kwamba mtu ambaye hajaokoka, huko huru kufanya chochote na kufanya lolote na yeyote. Yaani akitaka kuzini, kuiba, kudanganya, kujichubua, kujipamba, kutoa mimba, kutongoza, kujichua, yaani HANA MIPAKA wala HANA SHERIA inayomuwekea VIGOGO.

Lakini swali ni, hizo wanazoita Raha, miaka kadhaa baadae zitawapa matokeo gani?? Zitawafanya wawe nani, wenye sura gani na wenye maisha gani??

Miaka 20 au 40 baadae, ambaye hakuokoka na alikuwa ana uhuru wa kufanya atakacho kwa uhuru, atajikuta kwenye matokeo mabaya ambayo hata yeye mwenyewe hatajifurahia.

Upande wa wokovu huku ni tofauti, wenyewe ni umejaa MAKATAZO, MIONGOZO, SHERIA, VIGOGO. Yaani ukipiga hatua mbili mbele utakutana na hili hapana, umejaribu lingine unakutana na tangazo tena.

Mara huruhusiwi kuchati na mtu wa jinsia tofauti, mara kanisa hili tunakagua simu na kujua mawasiliano yako ya sirini, mara usitongoze binti yeyote hata kama unataka kumuoa kamuone mzee wa kanisa, au mama mchungaji au jaza fomu. Mara, ukiwa na mchumba usiwasiliane naye na wala usiongozane naye popote mpaka mkishafunga ndoa. Usinywe kile, usile kile, siku nyingine utafunga, ibada ndefu n.k.

Kwahiyo mwisho wa siku aliyeokoka anakuwa kama "MTUMWA" fulani hivi kwasababu haishi kwa "UHURU WA DHAMBI". Yaani daima anayo sheria inayomkataza asitende dhambi.

Maisha haya yanaonekana wazi kuwa ni ya MATESO (kwa mtu ambaye hajazoezwa/hana ufahamu sahihi) na ni kwasababu hiyo, wengi wa wanadamu hawayapendi maisha haya ya kuokoka na kumaanisha kwa Mungu.

Mtu huyu aliyeokoka miaka 20 au 40 baadae, baada ya kuumia na mifungo, mikesha, na ibada nyingi, anajikuta ana sifa njema kuliko watu wote kwenye jamii yake. Hazini, haibi, hatukani, ni msafi, hana SKENDO (makando-kando), akili yake iko safi, ujana au ubinti wake ameutunza, anajivunia kuwa hivyo alivyo. Yaani kama ni kijana basi mabinti wanasema nani anipe kuolewa na kijana yule na kama ni binti vijana wanasema nani anipe kuoa binti yule.

Ukweli ni kwamba FOCUS yao kubwa haiwi tu zinaa, bali wanakuwa wanaona UTULIVU WA HUYO MTU KWA MUNGU na wanaamini kwamba ni mtu salama sana kuishi naye.

Kama umesoma vizuri utakuwa umegundua pia kuna UJINGA FEKI na UJINGA OG. Yaani ambaye hajaokoka anamuona kama aliyeokoka ni mjinga, lakini kumbe yeye mwenyewe ndiye MJINGA ORIGINAL sasa.

Matokeo ya maisha ambayo anayaoshi mtu ambaye hajaokoka ndio yanayojulisha kwamba mtu huyu ni mjinga original. Sema tu jambo moja ni kwamba, saa ambayo anakuwa anaishi maisha hayo anakuwa hajui atakutana na matokeo gani baada ya maisha hayo.

Unasubiri nini KUFANYA MAAMUZI YA KUOKOKA?? Kama bado haujaokoka ama haujamaanisha kwa Mungu, saa ya wokovu ni sasa.

Nipigie kwa namba 0714483548
Mch. Helbeth Mlelwa
Dar es Salaam

84 - 8

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 month ago

Asilimia kubwa ya walokole hawawapendi ndugu zao, kwa kuwa wanaacha kwenda kuangamia kwenye jehanamu ya moto huku wakiwahubiri watu wa mbali kwa machozi.

Hebu jiulize maswali haya; wakati wewe unahubiri sana injili mtaa kwa mtaa tena kwa kuwaambia watu kwamba maisha ya dhambi yatawagharimu, je ndugu zako unawaambia ukweli huo kwa lugha kama hiyo unayoongea mtaani??

Yesu aliwahi kutoa mfano wa maskini Lazaro na yule tajiri, je wewe unaamini ule mfano ni wa kweli? Kama mfano ule ni wa kweli ni lazima uwe unajua kwamba siku moja utamuona mama yako au baba yako, dada yako au kaka yako akiwa "ANATESEKA" kwenye jehanamu ya moto.

Swali ni; Hawa dada zako na kaka zako walikupenda sana mkiwa duniani na walikusaidia mambo mengi ila wewe haujawaambia habari za ufalme kwa uzito uliotakiwa na ndio maana HAWAJATUBU na kwasababu hiyo UTAKUWA unashuhudia wakiwa WANATESEKA milele na milele?? Je mpaka hapo wewe unawapenda ndugu zako kweli??

Kabla hatukaenda kwenye eneo la kuwaombea au kufunga kwa ajili yao tubaki kwanza kwenye eneo la kuwaambia tu. Kwasababu Yesu alisema kama wasipowasikia hao manabii hata wakishuka wafu kutoka mbinguni bado hawataamini (yaani wanaweza kusema ni uchawi wala sio Mungu). Katika hao manabii na wewe umo humo ndani ila hauwaambii uhalisia ndugu zako.

Wengi wa tuliookoka na kumaanisha (tunaijua dhambi ni nini) wazazi wetu bado ni walevi, waongo, wana michepuko n.k. Je, kwa maisha hayo hawataingia jehanamu ya moto.

Je umewahi kuwaambia ndugu zako ukweli ulionyooka kwamba hayo maubatizo ya watoto wanayoyafanya, sakrament za kipaimara, kusali rozari/kumwomba bikira Maria awaombee kwa Mungu, kuwaomba watakatifu wawaombee, na mengine mengi ni ya kishetani na hayapo kibiblia??.

Je umewahi kuwaambia ndugu zako kwamba kama anaenda kwa mganga wa kienyeji hilo ni kosa kubwa sana kwasababu Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu, kwa kosa hilo Mungu alimuua Sauli lakini leo hii watu wanachukulia kawaida tu.

Kama kuna ndugu yangu unasoma hapa, nakusihi sana kwa huruma za Bwana wetu Yesu Kristo, OKOKA na UACHE DHAMBI ZAKO zote za hadharani na za sirini. Safari ya kifo ii karibu nasi, tubu haraka kwasababu ukikata roho hakuna kuokoka tena, wokovu ni ukiwa hai, ukishakufa wewe unasubiria kwenda kutoa hesabu ya matendo yako.

Ukisoma ujumbe huu dada yangu, kaka yangu au yeyote yule ambaye hujaokoka, narudia tena, safari ya mauti ii karibu nasi, tubu dhambi zako na uokoke haraka. Acha ubishi, wa kusema umeokoka wakati maisha yako machafu unayajua na dhamiri yako inakushuhudia kwamba ukifa leo MBINGUNI huingii.

Najua mnajua ni kama natania, ila mimi sijui nini kipo mbele yangu, kuna shida imejitokeza ghafla kwenye mwili wangu, lakini sio tatizo kubwa, ila cha ajabu leo usiku nimekosa usingizi na kwa namna isiyo ya kawaida, Mungu amenipa kulia sana, hata nikitoka nje natembea ila bado naona nalia, hadi nikaanza kumuuliza Mungu kwani kuna nini mbele yangu??

Najua wa kupuuza mtapuuza kama kawaida yenu, ila nikiwaona mahali mpo mnataabika kwasababu ya kutokutubia maisha yenu, nitamwambia Mungu nilitomiza wajibu wangu tena kwa machozi.

Kama kuna ndugu yangu au yeyote unataka kuongozwa sala ya toba nipigie 071448354835

@highlight Florentina Mlelwa Christer Mlelwa Flaviana Mlelwa Frument Mlelwa Frument Mlelwa Florentina Mlelws Flaviana Mlelwa William Issack Dionis Izack

70 - 18

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 month ago

KISA CHA NYOKA WA MAAJABU

Nyoka huyu anaishi kwa kutegemea nyoka wadogo wadogo ambao huenda huku na kule kuwatafuta jamii ya watu wanaopinga mwenendo wa nyoka huyu ili wawaue na hatimaye nyoka huyo anainywa damu ya wanadamu hao na kisha anatema asali na kutaka wanadamu waipokee na wamkubali. Je wewe waweza kuipokea na kuilamba asali inayotemwa na nyoka huyu?

2.Waweza kufanya urafiki na nyoka huyo?

3. Waweza kumpongeza nyoka huyo?

Yeyote ulivyoelewa ni uelewa wako ila mimi nimeuliza swali kuwa je, waweza kuipokea na kuilamba asali ya nyoka huyo?

Mimi nitampinga nyoka huyu kwa dua, sala na namna nyingi Mungu amuue kwa njia yoyote

27 - 10

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 month ago

FUATILIA IBADA YA MKESHA KWA LINK IFUATAYO
youtube.com/live/qg6AHuXw_cE?si=KAqmHtJGAQaerFGb

51 - 4

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 month ago

KIJANA MWENYE MALENGO YA KUTEMBEA NA MUNGU KWA SAFARI NDEFU, UNAHITAJI CHAKULA CHA KUKUSAIDIA.

1. Unaitaji uelewa imara na thabiti usioyumbishwa kirahisi
2. Unahitaji kujua upatikanebsana wapi?
3. Unahitaji kujua vipaumbele unavyotakiwa kuwa navyo.
4. Marafiki unaotakiwa kuwa nao n.k

Yote hayo yapo ndani ya video hii; https://youtu.be/Aw61QTCvwF0

Yeyote atakayefuata mafundisho ninayofundisha na ninayoyaishi naamini atakuwa miongoni mwa vijana watakatifu sana kwenye dunia hii iliyooza na kunuka DHAMBI, ndio, unaweza kuwa mtakatifu.

Helbeth Mlelwa
Dec 26, 2024

36 - 0

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 1 month ago

SITAKI MTU ANITAKIE KHERI YA KRISTMASS WALA MWAKA MPYA (Hakuna sherehe yotote katika siku hizo mbili).

Mwanafalsafa wa mbinguni Helbeth Mlelwa, Dec 24, 2024.

Kwa haraka haraka unaweza kudhani huyu jamaa ana misimamo ya kitoto sana au "HANA SHUKRANI" kwa "MUNGU" au ana kiburi cha uzima, lakini ukifuatana nami sawa sawa unaweza kujikuta huenda hata wewe hauna mwaka mpya, ila tu kuna wahuni fulani waliotunga kalenda ndio walikwambia uwe unasherehekea, sasa kaa chini jaribu kujiuliza, huwa unasherehekea kwasababu gani??

Unapika mivyakula ya gharama, unatumia pesa nyingi, unanunua mavazi, kama ni mlevi unalewa pombe, kama malaya unazini sana. (Kwa malaya na walevi, wao wanasherekea kwa kupata nafasi ya kuendelea kuishi kudiani ili waendeleze umalaya wao, kwa kuwa baada ya maisha haya hakuna umalaya tena), lakini wewe MWANA WA MUNGU, unasherehekea kiti gani?

Mwaka mpya ni kubadilika kwa hali ya mambo. Wana wa Israeli walikuwa wanaita mwaka mpya baada ya Bwana kugeuza uteka uliokuwa juu yao. Yaani kwa mfano hawa wanaotekwa, kuuwawa, kuumizwa, kuteswa, kudhulumiwa, wote wakitoka kwenye hali hizo, hapo ndio mnaweza kusherehekea mwaka mpya.

Kwa hali tuliyonayo sasa hapa tulipo. Unasherehekea mwaka mpya kwa lipi? Kimebadilika nini?. Unamwambia mtu kheri ya kuongeza miaka ya kuteseka au unamwambia kheri ya nini sasa??


Ngoja nikupe mfano huu rahisi. Hivi unafikiri wazazi wa vijana waliotekwa na kupotezwa kama Shadrack (aliyechoma picha ya rais) au akina Deusdedith Soka, wao wanaona furaha/sherehe yoyote kwenye huo mwaka mpya??. Wao wao na tafakari zao kubwa, ni lini tutajua watoto wetu wapo wapi na wana hali gani?. Kwenye mazingira hayo hakuna pilau inayolika wala hakuna soda inayonyweka, yaani nguvu ya hilo wazo ni kubwa kuliko hizo kelele zinazoitwa sherehe.

Sasa kuna mtanzania mwengine na wewe upo kwenye line ya kutekwa au kupotezwa halafu unakaa chini unasherekea mwaka mpya, hivi wewe unakuwa unautimamu kweli?? Najiuliza kwasababu, katika hali ya hatari watu huwa hawasherekei hata siku moja. Swali la kwanza Gidioni alipotokewa na Bwana alimuuliza, yako wapi yale matendo yako makuu tuliyoyasikia/tuliyosimuliwa, maana yake hiyo ilikuwa ni tafakari ya Gidioni siku zote.

Anyway, Mwaka mpya mimi nitasherekea pale nitakapoona Bwana amebadili uteka wetu, vinginevyo msinisumbue mimi na hizo kelele zenu, eti kheri ya mwaka mpya.

Mimi mwenyewe nitamshukuru Mungu kwa kunipa uhai, ila nitamshukuru nikiwa natafakari, kwanini miaka inaongezeka halafu bado niko utumwani ndani ya nchi yangu mwenyewe.

Ila kelele zenu za kheri hizo sijibu, sasa wewe jifanye huna akili. Hata ukikutana na mimi popote usinitakie kheri mimi.

Kama Mungu akiruhusu niendelee kuishi nitaishi kwa kuwa (1) Siwezi kujiua lakini jambo la pili (2) Inawezekana ananiacha niishi ili niongezee jitihada na bidii kwake ili hatimaye atokeze ukombozi wa milele kupitia mimi kwenye nchi hii na dunia kwa ujumla.

Lakini ukweli ni kwamba unayefurahia miaka inazidi kuongezeka upo duniani, dunia kama hii, huna tafakari yoyote ya mambo yabadilike, wewe ni zaidi ya mwehu. Kwasababu hii duniani inakoendelea kwenda, hata wewe mwenyewe usipokaa sawa utasombwa na hii kasi ya dunia au watakuteka na kukuua tu (haina cha wewe ni mchungaji wala nani).

Dunia ina kasi ya hatari sana na ndio maana leo unasikia mwimbaji wa nyimbo za injili anasagana na bado anaendelea kuimba. Wewe unafikiri dunia inaenda wapi??. Wewe unafikiri duniani kwasasa dhambi ni nini??. Kama makosa ya sodoma na gomora ambayo Mungu akiangamiza watu, sasa hivi yanafanywa na waliookoka na bado wameokoka, hapo wewe unaona tunaelelea wapi??

Ukifurahia kuendelea kuishi kwenye dunia hii, sijui unafurahia nini?? Kwasababu hata mali, utajiri, ukwasi utakaotafuta, vyote utaviacha hapahapa duniani, wewe utaenda na nafsi yako kusimama hukumuni.

Sasa unafurahia nini kuendelea kuwepo duniani??

71 - 30

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 2 months ago

MOJA KATI YA KOSA KUBWA LINALOWAUMIZA NA LITAENDELEA KUWAUMIZA VIJANA WAOWAJI NA MABINTI WAOLEWAJI NI "MATARAJIO AMBAYO HAYAPO"

Kwa maana rahisi ni kwamba kijana muoaji anakuwa ana matarajio yake juu ya binti anayemuoa, na binti muolewaji anakuwa ana matarajio yake juu ya kijana anayeolewa naye, na kwa bahati mbaya sana "mara nyingi" matarajio hayo huwa hayako hivyo.

Bahati mbaya nyingine ni kwamba wengi wao huwa hawajipangi kisaikolojia "kupambana na changamoto" bali huwa wanajipanga kisaikolojia kwenda "kufurahia ndoa" sawa na "waongo wengi" walivyowadanganya huku nje kabla hawajaingia kwenye ndoa.

Sambamba na hilo, ni vema ufahamu kuwa maisha ya kijana huyo au ya binti huyo unayoyafahamu au utakayoyafahamu kwa uchunguzi wowote ule, ni asilimia ndogo sana ya uhalisia wa maisha yake. Yaani ni sawa na kumjua mtu asilimia 25% kati ya 100% na kuamini huo ndio uhalisia wote wa maisha yake. Ila utakavyomuoa au kuolewa naye utaenda kuishi na asilimia 100% ya huyo uliyemuoa au kuolewa naye.

Hii huwa inaleta challenge (CHANGAMOTO) kubwa inayopelekea mwanandoa huyu aone duniani panaanza kuwa mahali pa moto, baada ya kuona matarajio yake hayako vile tena katika uhalisia aliokutana nao.

Ee mtu wa Mungu, kabla hujafanya maamuzi ya kuoa au kuolewa zingatia mambo yafuatayo;

1. Kuwa mtulivu, usiwe mkurupukaji au mwepesi wa kufanya maamuzi. Yaani tambua kuwa ndoa ni taasisi inayoweza kuja kuzaa faida ikianza na "kutofautiana" katika mengi na "kupangana" katika mengi.

Kutofautiana huku kunatokana na utofauti wa malezi yetu, haiba zetu, makuzi yetu n.k, lakini lengo la kupangana ni ili wote twende kwenye nia moja.

Ni kweli kwamba kanuni inayotakiwa kumwongoza mwanamke ni KUTII na kanuni inayotakiwa kumwongoza mwanaune ni KUISHI NA MKEWE KWA AKILI. Hii ni kwasababu, ni jambo gumu sana kumtii mtu unayeona wazi kabisa kwamba anakuongoza kuelekea shimoni, hapo lazima utakataa na utakuwa umeshindwa kuwa mtii.

Mtihani ndio unaanzia hapo sasa, na ndio maana huwa tunashauri kijana asimuoe binti aliyemzidi umri. Hii ni kwasababu, akili huwa inatokana na mambo mengi uliyowahi kukabuliana nayo na kuyatatua bila kumuumiza mtu. Ujumla wa mambo hayo huzaa AKILI ambayo ikimuongoza mtu na akaona katika kila unalomuongoza haumii, ndio chanzo cha utii wa mwanamke.

Vichwa vya wanadamu vina mambo mengi sana ambayo vinaamini kwamba ndio yapo sahihi zaidi. Akili yako isikuambie kwamba kama kijana utaoa tu binti na kirahisi rahisi tu ataanza kufuata mitazamo yako, bila yeye kuona hiyo mitazamo yako imewahi kuzaa faida wapi na wapi??. Ndio maana msemaji mmoja aliwahi kusema kwamba KAMA HUNA AKILI USIOE kwasababu biblia imemuagiza mwanamume kuishi na mwanamke kwa akili, lakini kama kijana wa kiume huyu anakuwa hana akili ni afadhali asioe, utazaa magomvi mengine.

2. Jiandae kisaikolojia kukutana na changamoto au mlima na wala sio mteremko. Najua ni kweli baadhi yenu mnaweza kunipinga, ila mimi sijawahi kuamini kama kuna binti yeyote duniani unaweza ukamuoa au kijana yeyote duniani ukaolewa naye na ndoa ikawa "mteremko" hasa kwa siku za mwanzo, huyo hayupo wala hatakuja kuwepo mpaka dunia inaisha.

Maana yangu ni hii, kama ni binti kufuata mitazamo ya kijana, huo ni mlima, kwasababu sio jambo rahisi kuweka mambo yako chini na kufuata ya mtu mwingine. Amini tu kwamba itakuchukua muda kuwa na utayari huo na kuyafuata hayo kwa kipimo cha kumfurahisha mumeo. Hali kadhalika, kijana utakuwa na mlima wa kumwelekeza huyo binti sababu, maana na faida za yeye kufuata mitazamo yako na hasara za mitazamo aliyonayo ikilinganishwa na ya kwako.

Huu ndio mlima ambao kila mwanandoa mpya lazima aupitie kabla hajaenda kuwa na ndoa yenye manufaa kwenye jamii yake.

Ni kweli kwamba, ucha Mungu au kupondeka kwa mioyo ya watu hawa kwa Mungu, inaweza kuwa ni sifa itakayopelekea mlima huu usiwe mrefu sana kuupanda, lakini kwa bahati mbaya sana, hao waliopondeka mioyo yao kwa Mungu ni vigumu sana kuwapata kizazi hiki. Ndio maana mtu amekosana na mke wake wa ndoa wazo la haraka haraka ni kwamba hata tukiachana nitaoa mwingine.

Hoja sio kuoa mwingine. Hoja ya kwanza ni kwamba huyo uliye naye tayari una agano naye na mmeunganishwa kwa agano. Lakini hoja ya pili, kwa akili yako unafikiri huyo utakayemuoa ndio atakuwa perfect (amekamilika)?? Jibu ni hapana.

Uko ufahamu wanadamu walitakiwa wawe nao kabla hawajajiingiza kwenye baadhi ya mambo. Wawe wanajua watakutana na changamoto zipi na wajipange kukabuliana nazo, vinginevyo UTAUMIA.

Mch. Helbeth Mlelwa
Dar es Salaam
17 Dec 2024; 16:00

70 - 18

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 2 months ago

Kumeibuka system moja hivi sasa ya kishetani sana.... madhara yake yako kwenye upande mzuri kwa jicho la kawaida. ila hii system ni ya kishetani kabisa.

Mtoto anaondoka nyumbani usiku anarudi nyumbani usiku anaenda shule jumatatu hadi jumapili..... mtoto huyo ni darasa la 7

Mtoto anahaki ya kupumzika, watu wa haki za binadamu mkowapi? watoto wanafanyishwa mental work full time 14/7.

Unajua ukitaka kuua taifa lolote... wewe ua dhamiri za watu wa hilo taifa...watakuwa tayari kuua wakati wowote na mtu yeyote, watakuwa wezi wasio na hatia, watakuwa na ukatili na roho mbaya za kila aina.

Sasa haka ka system ni kama kamelenga kuwasaidia watoto. Ila kana makusudi mabaya sana, jiulize watoto watafundishwa maadili ya kuwa na hofu ya Mungu saa ngapi?? Huyo mtoto akija kuwa shoga yeye atakuwa anaona kawaida, atakuwa anaiba anaona kawaida kwa sababu hana hofu ya Mungu.

Sasa ni kama wanataka kuwasaidia watoto lakini hakuna kitu..... hata mashine zinapumzika.....mtoto wa darasa la 7 anasoma siku zote za wiki jumatatu hadi jumapili kuanzia asubui mpaka saa 4 usiku mwaka mzima. Utaniambia kunavitu vinaingia kichwani au anakuwa amekalili tu.

Mtoto muda wote amechoka akikaa kidogo tu anaanza kusinzia.

Wazazi tushirikiane watoto wetu ni bora kuliko izo A ambazo hazina kazi wanazotaka wanafunzi wazipate.... mimi nimefika hapa na kupata degree yangu sijawai kupata A NECTA na chuo nimefika.

Hivyo bora wakose A ila wawe na maadili......tuzipinge kwa nguvu moja hizi shule za kwenda hadi jumapili....wanaenda kufundishwa na mwalimu mzinzi, mwalimu malaya, wawalimu walevi....... wewe unadhani kuwa ataambiwa nini akienda uko shuleni.....

Wakristo wenzangu tuamke shetani anawakamata watoto wetu na sisi tunaona kawaida..... atakapokuwa shoga au malaya ndio utaanza kusema unapigwa vita..... kumbe ulijipiga vita mwenyewe.

Vitoto vyenyewe vinavyomaliza kichwani vinakuwa havina kitu ila vimemeza tu manotes...... ukikatega kidogo tu kanabaki kanakutolea macho hii ni ishara hata wakisoma hadi jumapili hakuna kitakacho badilika.

Sisi hatukusoma hadi jumapili ila tulifaulu vizuri tu.....

Mtoto anatakiwa apumzike ni haki yake ilo sio ombi, mtoto sio mashine.... ata mashine huwa tunazipumzisha.

Regard
Engineer Anord Amri
Mtumishi wa Mungu

126 - 50

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 2 months ago

NIKO MBIONI KUTANGAZA MAOMBI MAALUMU YA KUMWOMBA MUNGU ASIMAMISHE UTAWALA WA HAKI TANZANIA ( yaani UTAWALA UTAKAOZINGATIA UTU NA UBINADAMU ZAIDI na sio KILA MTU KUJALI CHEO CHAKE AU YEYE APATE NINI, HATA KAMA ATAMUUMIZA MWINGINE).

Helbeth Mlelwa, December 3, 2024; 01:08

Shalom (amani iwe nanyi) watu wa Mungu wote mnaofuatilia ukurasa huu. Lakini pia mnaofuatilia machapisho yangu kwa ujumla.

Nimeona niandike maelezo haya mapema kabla sijayaelezea kwa njia ya clip, ili yeyote utakayeweza kuendelea kujiandaa, uendelee kujiandaa.

Kiufupi nieleze kuwa, kwa mtazamo wa ki Mungu, uhalisia wa hali ya kiutawala iliyowahi kuwepo na itakayoendelea kuwepo Tanzania, itazidi kuwa mbaya siku hata siku. Hii ni kwasababu inaonekana ni aina fulani tu ya watu (walio kwenye chain au kikundi fulani) ndio ambao wana UHAKIKA wa kugombea na WAKASHINDA UCHAGUZI na wakishashinda kwa njia hiyo wanatawala watakavyo wao, kwa kuwa wao hawashughuliki na waliowachagua bali wanashughulika na kuponya, au kuyaangalia sana maisha yao huku wengi wa raia wa kawaida tukiishia kulia KILIO CHA SAMAKI, kisichosikilizwa na mtu yeyote.

Ni kweli kwamba wako watu wanaweza kuonekana ni kama wanasikiliza vilio mnavyolia na ni kama kuna matamko yanatolewa, ila mwisho wa yote mtashamhaa sana kwamba hali ya mambo haibadiliki hata kidogo.

Amini nakuambia, hapa tulipo, hatuhitaji KATIBA MPYA, wana hatuhitaji CCM itoke madarakani, ili kiingie chama kingine kama CHADEMA au chochote kile. Nakufafanulia kwa ufupi sana ni kwanini nasema hivyo;

(a) Hatuhitaji KATIBA MPYA kwasababu, hata hii katiba iliyopo, watawala WANAIKANYAGA na hakuna wa kuwafanya lolote. Hiyo ni ishara ya wazi kwamba KATIBA si kitu "CHENYE NGUVU" ya kumfanya mtawala awajali watu wake au ajali maisha ya watu wengine.

(b) Hatuhitaji CCM itoke madarakani kwasababu, unafikiri CCM ikitoka madarakani, CHAMA GANI ndio kitafaa kuongoza??. Kama unatumia akili yako timamu hebu waza jambo hili mara moja. Ikiwa kiongozi wa chama fulani cha siasa X, anaweza akawa na mchepuko (aidha ni kabinti au mke wa mtu), unadhani anayeweza kuzini na binti au mke wa mtu ambaye si mke wake, ataogopa kupanga UTEKAJI au mauaji kwa mtu fulani??

Kama mngekubaliana nami ni kwamba hiki kinachoonekana kama upinzani na chama tawala kwa nchi kama Tanzania, ni danganya toto tu, ndio maana huwa unaweza ukafika wakati ukaona mwanasiasa kahama chama X kwenda chama Y cha siasa kwasababu tu kule chama X amekosa nafasi ya kugombea au kuna favour (upendeleo) flani ameikosa. Hiyo ni lugha tosha kwamba asilimia 99.9 ya wanasiasa wanatafuta ulaji tu na wala sio watu wanaoweza kutetea watu kweli kweli.

Vyama vya upinzani vinavyoota ndoto ya kuja kuitawala Tanzania, vinaota ndoto NGUMU SANA ambayo haina mahali pa kupita kwenda kutokea huko.

Nawahakikishia kwamba hata tulipo kwenye hii nchi, TUNAHITAJI MAAJABU YA MUNGU TU, ili tutoke katika mateso haya tunayoteseka. Kumbuka nimekwambia, kwanza chama pinzani kushinda ni NDOTO AMBAYO HAINA PA KUPITA ili ikatokee, na mbili, hata wakishinda kwa asilimia kubwa, wengi wao watashughulika na maisha yao tu kwasababu siasa ni kama kamchezo ka kutupiana maneno huku vita vya panzi furaha kwa kunguru (wazungu wanaotaka raslimali zetu).

Tawala na watawala wengi kwa sasa ndani ya Afrika, ili wapate utawala lazima wasaini makubaliano na hiki chama kinachoitwa FREEMASONRY ambao kimsingi wana mipango mikakati ya kuitawala dunia, na miongoni mwa njia wanazoweza kuzitumia ni kuwatesa sana watu ili wamsujudie mnyama (Al-Masih ad-Dajjal).

Niseme kwamba, mimi hapa siongelei siala la CCM au CHEDEMA ndio itawale, wala sishughuliki na mkristo au mwislamu atawale, nashughulika na ATAWALE MTU WA MUNGU, yaani mtu ambaye ATAITIISHA NCHI yote kwenye sheria hii moja kuu, LILE USILOPENDA KUTENDEWA WEWE, USIMTENDEE MWINGINE.

Mtu ambaye atagawanya raslimali zote za nchi kwa usawa kwa kira raia na kila raia atamshukuru Mungu kwa kuumbwa na kuzaliwa ndani ya nchi ya Tanzania.

Ndio, hiyo inawezekana sana. Mbona akina Ghadafi kwa kutumia mafuta tu yaliyoko Libya waliweza kulipa mishahara hata kwa wasomi ambao hawajaajiriwa, kujengea watu nyumba, kununulia magari kwa kuchangia gharama nusu, kila mama mjamzito anayejifungua kupewa pesa n.k. Nchi kama Australia ukiwa raia yeyote yule, kuna pesa ya kula kila mwezi unapewa, yaani maana yake wanakutengenezea mazingira usife njaa wewe wala watoto wako.

Najua ni wazo humu kukubalika kwasababu swali kubwa linakuwa, kwahiyo huyo mtu atapatikanaje au atafikaje kuwa kwenye uongozi kama atakuwa hana chama??

Jibu ni! ATAINULIWA NA MUNGU. Mimi naamini Mungu ni mamlaka yenye nguvu sana iliyowahi kumfanya Farao ashike adabu. Mahali pengine Nebkadreza alishika adabu kwa kwenda kula majani ya ng'ombe kondeni. Je, si zaidi wanasiasa hawa wa sasa ambao wamejieneza kwama mwelezi wa Lebanoni??

Nchi hii SIO MALI YA WANASIASA, na kama Mungu aliwahi kusikia kilio cha watu wake walioomba, basi na sisi tunatakiwa kuomba mpaka Mungu asikie na akomeshe jeuri na kiburi cha watawala hawa. Atakomeshaje, hilo sio suala la sisi kushughulika nao kwa kuwa tumeshaongea ila wao hawasikii. Pamoja na kwamba tutaendelea kuongea tena na tena, ila upande wa pili tuwekeze nguvu kwenye maombi mpaka Mungu asikie.

Awamu ya kwanza ya maombi haya yataanza tar 1 ya Jan 2025 na kuendelea hadi mwisho wa mwaka. Utakayeweza kufunga na kuwa unatumia chakula kidogo kila siku jioni, utakuwa umefanya ibada zaidi ya kumshawishi Mungu.

Maombi yatakuwa yanaombwa kila siku alfajiri ya saa 11 na kurushwa hewani live kwa channel yangu ya YouTube ya ‪@njiailiyonjema‬ . Popote pale utakapokuwa kwa muda huo, tamka neno juu ya nchi yako, tunaolia na kuumia ni wengi, tamka neno ili Mungu afanye jambo.

Kumbuka, hapa HATUOMBEI UCHAGUZI MKUU au ACHAGULIWE MTU SAHIHI. Nimekwambia kwamba MTU atakayetawala kwa haki, HAWEZI KUTOKANA NA SIASA HIZI ZA MANDUMILA KUWILI, hivyo huyo mtu Mungu akimwinua, ataingia ikulu kama ni kutokea kanisani au kutokea msikitini lakini sio kutokea kwenye vyama hivi vya siasa.

Ukweli ni kwamba kinachoitwa UCHAGUZI MKUU ni prosess za kupotezeana muda tu na ndio maana hata ukipita uchaguzi, utawaona bado ni wale wale watakuwepo madarakani. Ni lazima watu wa Mungu tuache kuombea uchaguzi, ila tuombee hali ya mambo kubadilika kwa asilimia 100%. Mungu anayo nguvu na uwezo huo.

Mwisho nimalize kwa kuseme; POST HII INAWEZA KUNIONGEZEA HATARI ZAIDI. Idara za kijasusi za dunia hii zinaweza kunipa kesi ya uhaini kwamba nataka kupindua serikali au nimetangaza kusudio hilo. Lakini ikumbukwe kwamba, lengo letu ni MTAWALA ATAKAYETAWALA KWA HAKI, hata kama watakuwa ni CCM hawa hawa na Rais Samia huyu huyu, ila Mungu ambadilishe moyo wake asiwe kama alivyo hivi sasa (hapo nitahesabu maombi yangu yamejibiwa).

Huenda wataanza kujiuliza huyu Helbeth Mlelwa ndio nani??. Lakini pia huenda wakimjua na wakaona ni mtu asiye na kigogo yeyote nyuma wala majeshi, wanaweza wakapuuza na kuona ni mpumbavu tu mmoja amerukwa na akili. Kanisa kwa ujumla wake linaweza kuanza kuangaliwa kwa umakini sana, na hata injili iliyonizaa na baadhi ya account nilizochapisha chapisho hili.

Najua kuwa, Mungu anaweza akajibu maombi haya au asijibu, akijibu inaweza kuwa nilifanya maamuzi ya kishujaa sana kutangaza hivi na kuanza kurusha maombi hayo kipa siku. Lakini Mungu asipojibu naweza nikaonekana ni kama chizi au nikadhaulika sana. Jambo moja ni kwamba, moyo wangu unaniambia, ni afadhari KUTUMIA NGUVU KUBWA KUMTAFUTA MUNGU hata kama hataonekana na ukaonekana ni kama ulikuwa kituko tu, bado una heri kuliko aliyejikatia tamaa.

Mimi naingia kuomba kwa kuwa ninaamini ENZI YA WAOVU INA MWISHO, na siombi kama kuigiza, bali naomba nikiwa nimemaanisha kwamba hivyo ndivyo ambavyo nilitaka itokee na kama mimi na waombaji wengine tutapata kibali mbele za Mungu, atajibu maombi yetu.

48 - 26

Kikosi kazi cha injili🎖
Posted 2 months ago

PICHA ZA KUMBUKIZI; MBARIKIWA MWAKIPESILE ALIPOTEMBELEA KAPUNGA MBALALI MBEYA 26 Nov 2024, kuwaimarisha washirika wake walioko huko KUENDELEA NA MUNGU kwa hali yoyote ile.

Unaweza kufuatilia ibada hiyo kupitia kiambato hiki www.facebook.com/share/v/187XsohFdM/

Maeneo mengine ambayo atapita ni Mafinga, Dodoma, Karatu-Arusha, Simanjiro, Moshi, Simiu, Geita, Nkome, na hatimaye kufanya ibada ya Kongamano, Kahama-Shinyanga kuliko na makusanyiko ya makanisa ya Kanda ya ziwa na wengine wa kutoka maeneo mbali mbali.

Endelea kubarikiwa na ziara hizi za Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile.

Repota wako; Helbeth Mlelwa

52 - 7