Kwa majina ninaitwa Silvano Joseph jina la sanaa ninaitwa CMPOO .. Caria yangu ni uchoraji ila pia nafanya music 🎵🎶 aina ya rap japo niliwahi kufanya muziki wa kuimba.. Mimi ni mzaliwa wa Arusha nina asili ya Kilimanjaro.. Tanzania. Ninaipenda asili yangu na ninamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniumba muafrika.. nilianza kuupenda mziki wa rap mwaka 1993 baada ya kuona rap ambayo sana sana inatumika na unabeba ujumbe unaokemea kitu moja kwa moja ndio maana ilitumika na hip hop emcees ambao walitumia rap kukemea na kuelezea jambo ambalo limefunikwa na watawala..