Imani Kuu ni chaneli inayokupasha habari njema zinazohusu Kanisa ambazo zinalenga kumjenga mtazamaji kiimani kupitia mahubiri ya Maaskofu, Mapadre, Mashemasi, Mafrateli, Makatekista, Masista na walimu.
Inakuletea simulizi mbalimbali za kukuimarisha kiroho, kiimani na kimaisha kama vile maisha ya watakatifu yanayotusukuma kutenda mema zaidi na kuchukia dhambi. Similizi hizi zinatupa nguvu ya kutokata tamaa, kuongeza bidii katika kumtafuta Mungu na kuwajibika katika kumtumikia Mungu.
Pia inakusogezea matukio mbalimbali kama Misa Takatifu, Ubatizo, Kipaimara, Ndoa, Upadrisho, Uimbaji na matukio mengine yahusuyo viongozi wa Kanisa.
Tafadhali Subscribe, Like, Comment na Share.