Karibu kwenye idhaa rasmi ya YouTube ya Joyce Meyer Ministries kwa lugha ya Kiswahili.
Joyce Meyer ni mojawapo wa waalimu halisi wa Bibilia ulimwenguni. Vitabu vyake vimewasaidia wengi kupata tumaini na urejesho katika Yesu Kristo. Yeye huongoza kipindi kwenye redio na televisheni " Enjoying Everyday Life" kinachoonyeshwa ulimwenguni kote.
Shauku ya Joyce kuwasaidia watu wanaoumia ndio msingi mkuu wa Hand of Hope, kitengo cha huduma kwa watu katika huduma ya Joyce Meyer. Huduma yetu kwa watu kote ulimwenguni inahusika na mipango ya lishe, matibabu, nyumba za mayatima na mipango ya kukumbana na biashara haramu ya binadamu.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu huduma ya Joyce Meyer, wasiliana nasi kupitia : kiswahili@jmmwo.org
Joyce Meyer Ministries KiSwahili