Magreth James ni mtumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji kutokea mkoa wa Kilimanjaro Tanzania.
Ni mzaliwa wa familia iliyokuwa katika misingi mathubuti ya kiroho iliyochangia kwa kiasi kikubwa Binti huyu kuutambua wito uliopo ndani yake na wakati wa kutumika kwake.
Magreth ameanza safari yake uimbaji mwaka 2019 na tokea wakati huo Mungu amekuwa akimtumia kuwabariki watu wake kupitia mashairi na sauti yake yenye Nguvu za Mungu.
Magreth ana lengo kubwa la kumtumikia Mungu kwa Roho na kweli ikiwa ni pamoja na kuendelea kuupa mziki wa injili Tanzania heshima na utukufu kwa Mungu.