Kusoma Aura
12 videos • 175 views • by Rakims Spiritual AURA Aura Ni Nini!? Wengi wamekua wakiskia tu kuhusu ulimwengu na nguvu mbalimbali alizonazo mwanadamu bila kuweza kuzitambua au kuzitumia hapa nitakujuza aina ya mojawapo ya Nguvu hizo ambayo ni Aura Kila kiumbe hai kinachoishi kwa kutumia Oxygen kuishi kina AURA Aura -ni mionzi au miale ama vivuli viliovyopo katika mwili wa kiumbe hai vinavyomzunguruka mwili wake mzima. Ama kwa kiswahili rahisi tunasema Aura ni mwanga au mvuke Unaomzunguka kiumbe hai na hii kwa wale tunaotembelea ulimwengu wa kiroho yaani (Astral Plane) tunafahamu sana. Kwa wale wasiojua Aura: Hii ndio nafasi nzuri kwenu kuweza kujua mengi yanayohusu Aura. Hapa Utafahamu Maana yake, Faida zake na jinsi ya kutumia AURA yako na wengine kuongoza maisha yako pia hii ni hatua ya kwanza kabisa kufahamu kuhusiana na aura SABABU NA FAIDA ZA KUSOMA AURA ZA VIUMBE WOTE: Faida ya kwanza inakusaidia kumfahamu mtu akiwa mbele yako dhamira yake. Faida ya pili inakusaidia kufuata mawimbi ya aura za watu na kuwafuatilia kwa yale wanayoyapenda na kuwajua wanataka kuzungumzia kitu gani muda huo hata kabla hajasema Ni kinga kutokana na maradhi ya kiroho mapepo na wachawi ikiwa umeifunga vema. Inakusaidia kujijua wewe ni mtu gani na kwa nini upo hapo na njia gani ufuate(Ukiingia ndani zaidi) Inakusaidia katika kubadili maisha yako kama kumjua mtu wa kukusaidia na wa kukuharibia Inakuongoza njia za kupita hata kama ni usiku wapi kuna watu wabaya na wapi kuna watu wema Inakupa nafasi ya kumjua mtu na tabia yake kuu.Kwa kifupi msaada wa aura kwa ujumla ni kukulinda na kukuongoza mfano wa kuita ni nguvu ya muujiza utaona mtu anamtizama mnyama mkali na kuwa mpole au mtu anaamrisha pepo toka akatoka ukajua yule pepo kaogopa yule mtu hapana kaogopa aura(Nuru) inayomzunguka muhusika muda huo. RANGI ZA AURA & MAANA ZAKE: Aura zipo Kumi ambazo zina kawaida yakuingiliana; kwa mtu ambae ni mgeni katika kusoma wengi huishia kusoma rangi moja tu ya ambayo ni rangi ya mvuke wa fedha wenye kuonyesha uhai wa kiumbe husika. lakini ukitizama kwa makini utaona rangi sahihi inayokuwa kwa muhusika NYEKUNDU Watu wenye Aura nyekundu ni watu ambao wana nguvu na wenye ujazo ndani yao, wao huonekana ni watu wapya wenye mtazamo mpya kila leo. Wanapenda sana chakula, kusafiri safiri na kutembea na kufanya mapenzi. Kitu Walichojiwekea Sana katika akili zao ni kumba atajaribu tena ni watu wa majaribio majaribio au onja onja kwa jina lingine. ” Kwa sababu wenye aura hii hujikuta kwenye mambo moto moto kwa sababu ni aura inayokaribiwa sana na mashetani ni watu ambao huwa wapo ress ress mara nyingi.... ni watu wenye kuchukia kirahisi rahisi tu, nahupandisha jazba kwa mambo madogo madogo tu. lakini kwa juu ni watu wenye kujitolea msaada wanapohitajika pia ni watu wasio na noma. Ni watu wenye nguvu akilini na ni watu wenye nguvu pia mwilini, na ni watu wasio ugua kirahisi rahisi. Kwa Sababu resi zao huwa kama ni mazoezi katika miili yao na kuwaweka presha zao vizuri mara nyingi huwa ni wenye nyota ya punda na ng'e Ni watu wanaopenda mambo ya kuonekana dhahiri na hawana time ya kufuatilia au kuamini mambo ya kiroho. Wenye Aura Hii Nyekundu ni watu wanaoboeka kirahisi na huama eneo hilo au hata thread kama umeweka akisoma kidogo anaachana nayo hawapendi kuwa bored ndio maana huwa ni onja onja, Wanapenda Kutafuta pesa na kustarehe kirahisi. Lakini Pia Ni watu wanaopenda kuanzisha mambo kwa kasi na kushindwa kuyamaliza. Lakini pia wakioziweka akili zao eneo moja hadi huwin hapo hapo, hufanikiwa sana na kupata utajiri mkubwa katika maisha yao lakini pale tu wanapojijua. Hawa watu hawapendi kuzungushwa zungushwa hovyo hovyo hawakawii kukuita mruga ruga au tapeli wavutie kwa kuwaambia vitu upesi upesi na mambo wanayoyapenda. Ni watu Ambao Hawaisikilizi wenzao na hawataki kupelekeshwa hovyo bora uwakwepe hawa chovywa chovya ila ukimjua mbwa Jina hakupi Shida. Rakims S.