KANUNI NA MUONGOZO KWA WAFUATILIAJI WETU
Baharia TV inamilikiwa na kampuni ya BAHARIA MEDIA GROUP LTD.
Hiki ni chombo rasmi kwa ajili ya kutoa habari ndani na nje ya Tanzania, Habari za kisiasa, kiuchumi, Kijamii na michezo, tunazingatia misingi ya uhariri katika habari kwa kufuata yafuatayo:
A. Kuripoti habari za ukweli
B. Kusaidia kurekebisha taarifa zilizopotoshwa ili kuwapa ukweli wafuatiliaji wetu
C. Kufuata misingi ya habari kwa kuripoti habari zenye uwiano na kutoa fursa sawa kwa pande zote
D. Kujiepusha na udini, ukabila au mambo yoyote yanayoweza kusababisha uchochezi
MUONGOZO KWA WAFUATILIAJI WETU
A. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake
B. Baharia TV ina uhuru wa kufuta maoni yasiyo na maadili au yenye matusi makali
C. Baharia TV ina uhuru wa kupitia maoni kabla hayajaonekana na watu wote
D. Baharia TV ina uhuru wa kumzuia mfuatiliaji aliyekiuka masharti asiweze kuona habari zetu au kuweza kuweka maoni
Mawasiliano:
0620400226